Mkuu
wa idara ya masoko na mwasiliano wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu akiongea katika halfa ya makabidhiano ya
vitanda na magodoro 50 kwa hospital ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kama
sehemu ya mradi wa benki hiyo ya miaka 20 ya kujali jamii.
BENKI ya Exim Tanzania leo imekabidhi
vitanda na magodoro 50 kwa Hospitali ya mkoa ya Mawenzi, mkoani Kilimanjaro.
Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka
jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali
jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa
kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.
Hospitali
na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa
katika hospitali za rufaa. Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa,
benki ya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga
kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini -
hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za
serikali katika mikoa 13 nchini kama sehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye
lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.
Hospitali
ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro ni hospitali ya kumi na moja kupokea mchango huu
baada ya hospitali ya serikali ya Sekou Toure ya mkoani Mwanza mwezi uliopita,
hospitali ya rufaa ya Morogoro mwezi Aprili, hospitali ya rufaa ya Mwananyamala
mkoani Dar es Salaam mwezi Machi, hospitali ya rufaa ya Bombo,
mkoani Tanga mwezi Febuari, hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya mwezi Januari,
hospitali ya Mount Meru, Arusha mwezi Desemba, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi
Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi
Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es
Salaam mwezi wa nane mwaka jana. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo katika
wodi ya wazazi na mgeni rasmi alikuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr.
Best Magoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...