NA Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kujadiana kuhusu namna bora ya kupata ufumbuzi wa kudumu wa kero ya ulipaji kodi ya mizigo kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Wingwi, Mhe. Juma Kombo Hamad (CUF)M aliyetaka kujua kama Serikali ipo tayari kuunda Kamati Ndogo ya Bunge kwa ajili ya kushughulikia mfumo wa ulipaji kodi za mizigo kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Katika sawli hilo Mhe. Hamad alieleza kuwa mfumo wa ulipaji kodi za kusafirisha bidhaa kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu kwamba unawakwaza na kuvunja harakati za biashara Zanzibar na hivyo kusababisha uchumi wa Zanzibar kushuka.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji, alisema kuwa Serikali hizo mbili zinaendelea kujadiliana ili kuona kuwa suala hilo linapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuongeza kuwa Serikali hizo hazijashindwa kutatua changamoto hiyo na hakuna sababu ya kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo.

Alisema chimbuko la malamiko hayo linatokana na kuwepo kwa mifumo tofauti ya kutathmini bidhaa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara hali inayosababishwa na viwango tofauti vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kulipwa kwa bidhaa ya aina moja kutoka nje ya nchi na kusafirishwa kwenda sehemu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...