SERIKALI imeanza kulishughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kwa
vitendo baada ya kutoa kiasi cha bilioni 40 kwa ajili ya kutoa maji
kwenye chanzo cha mto zigi kupelekwa kwenye vijiji mbalimbali ili kuweza
kuondosha kero hizo iliyokuwepo muda mrefu iliyokuwa ikiwafanya
wananchi kutumia muda mwingi kusaka huduma hiyo.
Hayo
yalibainishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele
wakati alipofanya ziara wilayani humo kutembelea vyanzo vya maji Amani
na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani.
Alisema
kuwa mpango huo wa serikali unakusudia kuhakikisha changamoto za maji
ambazo walikuwa wanakabiliana nazo wananchi hao kwa muda mrefu
zinamaliza ili waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa
maisha yao na jamii zinazowazunguka.
Waziri Kamwelwe alisema
hatua hiyo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John Magufuli
kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi zikiwemo za maji ili
kuhakikisha tatizo la kutokupatikana kwa huduma hiyo linaondoka kwa
watanzania.
“Ndugu zangu serikali tumetoa bilioni 40 kwa ajili
ya kushughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kutoka chanzo cha Mto
zigi kupita vijiji vyote hadi Muheza mjini huu ni mpango wa kuhakikisha
changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji Muheza tunaipatia ufumbuzi
wa kina “Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...