Na Leandra, Gabriel, Blogu ya jamii

Tanzania Global Learning Agency (TaGLA) ambayo inajishugha na mafunzo kwa njia ya mtandao nchini leo wameshiriki semina iliyoshirikisha nchi 15 duniani.

Huku Tanzania ikiwa nchi pekee iliyoshiriki barani Afrika kwa kukutana kupitia mtandao na kujadili masuala mbalimbali ya ukuaji wa miji huku Korea kusini wakiwa wenyeji wa semina hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa mafunzo ya mtandao Charles Senkondo ameeleza lengo la semina hiyo iliyoendeshwa na Profesa Heungsuk Choi kutoka Chuo kikuu Korea ni kuangalia mipango mizuri ya ardhi ya jiji na majiji kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye na hata kuleta mvuto kwa wawekezaji.

Ameeleza semina hiyo iliyokuwa inaendeshwa kwa njia ya mtandao wamejifunza kutoka Korea kusini katika kukua kwa miji na majiji hasa wakati huu ambapo taifa limejipanga kukua kiuchumi na upangaji wa miji.

Aidha amesema kuwa wataalamu mbalimbali wameshiriki na wanataraji hapo baadaye washiriki wachache wataenda Korea kujifunza kuhusiana na semina hiyo.Pia semina hizo zitaendelea hadi Agosti mwaka huu, hivyo wadau wajitokeze kujifunza na ametoa rai kwa wananchi kuhusu kubadilika na kujifunza kwani kwa sasa dunia imekuwa kama kijiji.Hivyo kupitia TaGLA wananchi wanaweza kujifunza na kuona ushindani wa kiuchumi kidunia.

Kwa upande wa Ignance Mchallo ambaye ni Mshauri wa mazingira kutoka Legendary International Ltd ameeleza na ameshauri katika kugawana madaraka na utekelezaji wa mipango hasa katika serikali za mitaa kwa kufanya kazi zao katika kukuza maeneo wanayosimamia.Ameongeza kuwa maendeleo na mazingira ni vitu vinavyoenda sambamba na lazima mazingira yahifadhiwe na kupangwa vizuri ili kuvutia uwekezaji na kuyatunza kwa matumizi ya kizazi cha baadaye.

Naye Mwanasheria mwandamizi wa NEMC Manchare Heche ameeleza kufurahishwa na semina hiyo na kueleza kuwa kama taifa lazima tujifunze katika kupanga miji na majiji na kuhifadhi mazingira hasa katika kipindi hiki ambacho taifa limedhamiria katika kukuza uchumi na mazingira hasa ardhi lazima yatunze kwa kuvutia wawekezaji na kwa manufaa ya vizazi vya baadaye na wananchi wapende kujifunza kwa njia ya mtandao kupitia TaGLA.

Mwanasheria wa Mwandamizi (NEMC)Manchare Heche akichangia mada katika mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15 leo jijini Dar as Salaam.
Wandau wa mazingira wakisikiliza mada mbalimbali katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliOhusisha nchi 15 leo jijini Dar as Salaam.
Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles Senkondo (katikati) akifafanua jambo mara baada ya mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15, leo jijini Dar as Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mazingira kutoka Legendary International,Ignace Mchallo na (kulia) Mwanasheria Mwandamizi (NEMC) Machare Heche.
Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles Senkondo akizungumza na mwatendaji mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mtandao ambao ulihusisha nchi 15,Mwenyeji ikiwa ni nchi ya Korea kusini leo jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)Mshauri wa Mazingira kutoka Leogendary Intanational, Ignace Mchallo akijibu maswali aliyoulizwa na wadau wa mazingira katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao ambao ulihusisha nchi 15,huku mwenyeji wao ikiwa ni Korea kusini leo jijini Dar as Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...