Na George Binagi-GB Pazzo, BMG Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania APHFTA, imeanza kutoa mafunzo kwa viongozi wa elimu mkoani Geita ili kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani humo. 

 Viongozi wanaopatiwa mafunzo ni pamoja na Waalimu 100 wa Malaria (Afya) kwa shule za msingi, Waalimu Wakuu 100 wa shule za msingi, Waratibu Elimu Kata 66 pamoja na Waratibu Elimu sita kutoka halmashauri zote mkoani GHeita. 

 Akizungumza juzi kwenye kilele cha mafunzo ya siku mbili kwa washiriki kutoka halmashauri za Nyang’hwale, Geita DC, Geita Mji pamoja na Chato, Kaimu Mganga Mkuu mkoani Geita Dr.Moses Simon ambaye pia ni Mratibu Malaria mkoani humo alisema hatua hiyo imelenga kufikisha elimu hadi ya shule ili kusaidia kushusha kiwango cha maambukizi ya Malaria ambapo takwimu za mwaka 2017/18 zinaonyesha mkoa huo ni wa pili kitaifa kwa kiwango cha juu ukiwa na asilimia 17.3 ukitanguliwa na mkoa wa Kigoma wenye asilimia24.3.

 Mratibu wa Afya kutoka taasisi ya APHFTA, Dr.Berezy Makaranga alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ushirikishwaji wa sekta binafi ya afya katika kupambana na ugonjwa Malaria ukilenga kusaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuwashirikisha wanajamii namna bora ya kujikinga. 

 Washiriki wa mafunzo hayo waliahidi kutumia vyema elimu na vitendea kazi ikiwemo bandokitita walivyopewa na kufikisha elimu ya kupambana na Malaria kwa wanafunzi pamoja na wanajamii na hatimaye kushusha kiwango cha maambuzi ya ugonjwa huo mkoani Geita. 

 Mafunzo hayo yaliratibiwa na Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHFTA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) na yanaendelea katika halmashauri za Bukombe na Mbogwe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...