WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuvumiliana na kustahamiliana ndiko kunakolifanya Taifa la Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao. 

Kadhalika, uwepo wa amani nchini si tu unatoa fursa ya kutekeleza majukumu ya kiuchumi na kijamii bila hofu bali pia ni sababu muhimu ya wenzetu wengine kutoka nje kuona fursa ya kuwekeza na kushirikiana nasi katika kujenga maendeleo ya nchini. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 28, 2018) wakati akizindua Umoja wa Kimataifa wa  Wabunge Wapenda Amani tawi la Tanzania (IAPP), kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni, jijini Dodoma.

Amesema amani na utulivu ni tunu kubwa sana katika jamii yoyote ile Duniani na Tanzania muda wote imeendelea kuenzi tunu hiyo iliyojengwa kwenye misingi imara kupitia waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu Shirikisho la Amani kwa Wote  (Universal Peace Federation (UPF), ambalo lilianzishwa kwa lengo la kumkomboa binadamu kutoka katika udhalili wa kukosa mahitaji muhimu. 

“Hili linadhihirika kupitia mipango ya shirikisho hilo ya kushirikiana na jamii nyingine katika kuimarisha sekta zenye kugusa maisha ya watu wengi kama vile kilimo, mazingira, afya, elimu, miundombinu na nyinginezo,” amesema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa tuzo ya Balozi wa Amani na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mbunge wa Tabora Mussa Ntimizi katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018 katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh, katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...