• Pia yazindua ushirikiano na VODACOM ambapo wateja wa MPESA wataweza kushinda dakika za bure, intaneti na bidhaa mbalimbali kwa kipindi chote cha kampeni.
Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini Tanzania leo umezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Wachezaji wote wa Tatu Mzuka kuanzia leo mpaka fainali, wataweza kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda milioni 300 ambapo kwa kila shilingi 500 unayocheza inakupa tiketi ya kushiriki droo siku ya fainali.
‘Mpaka sasa hii ndiyo kampeni inayosisimua zaidi kwa sababu hakuna ushindi mkubwa namna hii wa jackpot ambao ulishawahi kutolewa nchini Tanzania’ alisema Bwana Sebastian Maganga, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka
Kwa kuwa huu ni msimu wa kucheza na kushinda na marafiki, Tatu Mzuka kupitia droo ya Mzuka Deile wanatotoa fursa kwa mshindi kuchagua marafiki wanne ambapo kila mmoja atapewa 500,000 katika ushindi wa milioni 10 zinazotolewa kila siku.
Katika droo ya Jumapili, marafiki 5 kila mmoja atapata milioni 1 kutoka katika ushindi wa jackpot ya kila Jumapili. Siku ya fainali, mshindi wa milioni 300 atatoa milioni 1 kwa marafiki zake kumi ili kukamilisha timu ya ushindi ya watu 11.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati wakizindua ushirikiano na VODACOM, ambapo wateja wa MPESA wataweza kushinda dakika za bure, intaneti na bidhaa mbalimbali kwa kipindi chote cha kampeni pichani kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana,mbali ya kushirikiana huko
Tatu Mzuka wamezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Tatu Mzuka wamezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga Tatu Mzuka pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana wakionesha kombe wakati wa wakizindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga Tatu Mzuka pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana wakionesha jezi maridhawa wakati wa wakizindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...