Wengine 25 wajeruhiwa...Kamanda Polisi Mbeya aelezea ajali ilivyotokea
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
ASKARI 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),JWTZ 1 na Dereva wamefariki Dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.
Akizungumza leo kwa njia ya simu na Michuzi Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.
Amesema kutokana na mwendo mkali aliokuwa anaendesha dereva wa basi gari hiyo yenye namba T 755 BAB aina Scania alishindwa kumudu kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao
Amesema kuwa askari hao walikuwa wakitokea Igunga kwenda Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mafunzo mengine ya jeshi baada ya kumaliza mafunzo katika kambi ya Igunga.Amefafanua kuwa dereva wa gari hiyo naye amepoteza maisha na kwamba miili ya merehemu hao ipo chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Mbeya.
Amesema waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni askari 25 na wanne hali zao ni mbaya na sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya huku majeruhi waliobakia wakipatika matibabu katika hospitali ya JKT Mbeya kwani majeraha yao si makubwa.
Baadhi ya Askari wa JWTZ na JKT wakishriki kutoa msaada kwa Majeruhi waliopata ajali iliyotokea katika eneo la Kawetele mkoani Mbeya mapema leo mchana.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.ASKARI 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),JWTZ 1 na Dereva wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...