Na Woinde Shizza ,Mwanza
IMEELEZWA sababu kubwa inayosababisha mabinti wadogo kujiingiza kwenye vitendo vya kujamiana na hatimaye kupata mimba na ndoa za utotoni ni umasikini katika jamii wanazotoka.
Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa Kampeni ya Binti wa kitaa Angello George wakati akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya BINTI WA KITAA iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza .
Kampeni hiyo inakuja ikiwa ni siku chache toka Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsi ,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndungulile kueleza kuwa tangu Januari hadi Aprili Mkoa wa Shinyanga takribani mimba 18,000 za utotoni zimepatikana.
Hivyo amesema kampeni hiyo itahusisha mikoa yote ya Kanda ya Ziwa naitafanyika kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kwa lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba na ndoa za utotoni nchini.
"Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazosababisha mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,"amesema.
Ameongeza Binti wa kitaa imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 18 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani.
Amesema wanatarajia kwenda kuifanya kampeni katia mikoa zaidi ya 20 nchini huku ikiwa na ajenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa kitanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF) inayoendesha kampeni ya BINTI WA KITAA Angelo David George akiwa anazungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Mwanza,namna ya kuepuka mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni .
Wanafuzi wa shule ya Mwanza Sekondari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa kampeni ya BINTI WA KITAA Angelo George wa pili kushoto (Picha na Woinde Shizza,Mwanza)
Mmoja wa Wazazi alieyehudhuria katika uzinduzi huo, Bi Carol Nzogere akizugumza na wanafunzi





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...