Na Emmaenul Masaka, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amepokea shehena ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.milioni 100 kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika la KOICA.

Makonda amepokea vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam ambavyo ni Digital X-ray tatu, Ultrasound moja, Kabati la usalama wa viumbe (safety cabinet) moja, Mashine tatu za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto watoto njiti (baby warmer) pamoja na mashine ya utakitshaji.

Baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa Balozi wa Korea kusini Bwana Geum Young Song RC Makonda amekabidhi vifaa hivyo kwenye vituo vya Afya vya Sinza, Mnazi Mmoja na Mbagala ambako kuna uhaba wa vifaa. 

Kabla ya kupokea vifaa hivyo RC Makonda alifanya mazungumzo na Balozi huyo wa Korea Kusini na kuwasilisha ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo ya udaktari na uuguzi ambapo Balozi Geum Young Song amepokea kwa mikono miwili ombi hilo.

Makonda pia amemueleza Balozi ombi la kujengwa kwa kituo kikubwa cha upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi kwenye eneo moja ambapo pia Balozi amepokea ombi hilo na kumsifu RC Makonda kwa moyo wake wa kujali wananchi. 

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Geum Young Song amesema wametoa vifaa hivyo kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar es salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya na wataendelea kusaidiana na Serikali.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa makabidhiano ya shehena ya vifaa Tiba mablimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka serikali ya Korea Kusini kupitia shirika lake la KOICA.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Balozi wa Korea kusini,Geum Young Song (kushoto) akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda vifaa hivyo leo jijini Dar as Salaam.
Barozi wa Korea kusini,Geum Young Song (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda vifaa tiba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...