Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa shirika la mawasiliano Tanzania TTCL ,Juvenal Utafu amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2018 ngazi ya mkoa wa Mbeya (Dream Miss Mbeya 2018), kuhakikisha wanatumia urembo wao kama nguzo ya kuzifikia ndoto zao.

Meneja huyo amebainisha hayo baada ya Walimwende hao waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora ya mashindano hayo, kutembelea afisi za shirika hilo kanda ya nyanda za juu kusini kwa lengo la kutambua mambo mbalimbali yanayo husu TTCL, ikiwa ni pamoja na namna ya uhifadhi wa taarifa za watumiaji wa huduma za mawasiliano. 

Utafu amesema kwamba Ulimbwende ni moja ya njia za kuonesha mchango katika jamii, lakini hilo litafanikiwa ikiwa walimbwende hao watajitambua na kusimama vema katika nafasi zao. “Ni lazima mtambue ya kwamba mna deni kubwa kwa taifa, la kutoa mchango chanya katika nyanja mbalimbali, hasa katika hali ya sasa ya dunia ya utandawazi na mapinduzi ya sekta ya mawasiliano”, aliongeza Utafu. 

Kwa upande wake Meneja msaidizi biashara wa TTCL mkoa wa Mbeya Charles Mwita, alisema kuwa amefarijika sana kwa kauli mbiu ya mashindano hayo isemayo “urembo na kazi kwa maendeleo ya jamii”, na kuwapa changamoto walimbwende hao kwamba hawana budi kuitekeleza kauli mbiu hiyo kwa vitendo. 

Juni 29 mwaka huu ni fainali za mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yenye lengo la kumpata mlimbwende atakayevikwa taji la Mrembo wa mkoa wa Mbeya (Miss Mbeya 2018). Aidha mshindi huyo wa kwanza ataungana na washindi wengine akiwemo mshindni wa Pili na tatu kuuwakilisha mkoa wa Mbeya katika mashindano ya ngazi ya kanda yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao, kuwatafuta wawakilishi wa kanda ya nyanda za juu kusini katika mashindano ya urembo ngazi ya taifa. 

Mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yameandaliwa na redio Dream FM ya jijini Mbeya kwa udhamini wa TTCL Corporation, PII Limited, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Ally Rich Sanaa Arts Limited, Kalulu Safari’s Tours Co. Limited, Pepsi, Paradise Inn Hotel, Michuzi Blog, Michuzi Tv, na Dorcus Beauty Point.
Afisa huduma kwa wateja wa TTCL Corporation Bi Niva Mkwe akiwaelezea washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo.

Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa TTCL Corporation Juvenal Utafu akizungumza na washirki wa Dream Miss Mbeya 2018 walipomtembelea ofisini kwake Jijini MbeyaMeneja msaidizi-biashara wa TTCL Corporation Mkoa wa Mbeya Charles Mwita akiwaelezea washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...