Na Veronica Simba – Dodoma

Wataalam mbalimbali kutoka sekta ya madini nchini wameshiriki warsha maalum iliyotolewa na wataalamu kutoka Australia, kwa lengo la kujifunza uzoefu kutoka nchi hiyo ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta husika. Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alifungua rasmi warsha hiyo ya siku mbili, Juni 4 jijini Dodoma na kusema kuwa Tanzania inahitaji kujifunza zaidi kutoka nchi zilizofanikiwa katika sekta ya madini kama Australia, ili iweze kukuza zaidi mchango wake katika katika Pato la Taifa.

“Wenzetu Australia, sekta yao ya madini ina mchango mkubwa sana; zaidi ya asilimia 40 kwenye Pato lao la Taifa. Kwa hiyo, tunakutana nao kubadilishana uzoefu, ni namna gani wao wamefanya kuwezesha sekta husika kuchangia kwa kiasi hicho kwenye Pato la Taifa.”

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa, suala muhimu ambalo Wizara ya Madini inalisimamia ni kuhusu usimamizi wa rasilimali za madini. Alisema kuwa, lengo jingine la warsha hiyo ni kujifunza Australia imefanya nini katika kusimamia na kutatua migogoro kwenye sekta ya madini, ili Tanzania itumie mbinu hizo kutatua migogoro iliyopo kwenye sekta husika.

Biteko alitumia fursa hiyo kuiomba serikali ya Australia kuangalia uwezekano wa kuendesha warsha husika kwa wachimbaji wadogo nchini ili wapate maarifa ya namna bora ya usimamizi wa rasilimali za madini. Akizungumzia mchango wa sekta ya madini kwenye uchumi wa viwanda, Biteko alieleza kuwa, rasilimali za madini ni tegemeo kubwa katika kukuza uchumi huo.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya madini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
Mtaalamu wa Madini kutoka Australia, Rick Rogerson, akiwasilisha mada katika warsha ya wataalam wa madini nchini (hawapo pichani), iliyofanyika Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
Kutoka kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi David Mulabwa; Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania, Prof Shukrani Manya wakijadiliana jambo, wakati wa ufunguzi rasmi wa warsha ya wataalam wa madini nchini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), akijadiliana jambo na Mtaalamu wa Madini kutoka Australia, Rick Rogerson, muda mfupi baada ya Naibu Waziri kufungua rasmi warsha ya wataalam wa madini nchini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...