Na Leandra Gabriel, Globu  ya Jamii

TAASISI ya House Of Vision (VHV) inayojihusisha na ujasiriamali imejizatiti kutumia msimu huu wa sabasaba kuwasaidia vijana kutengeneza uchumi wao binafsi kutokana na ujuzi unaotolewa na taasisi hiyo.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo bi. Zena Mulokozi ameeleza kuwa taasisi hiyo inatoa elimu ya ujasiriamali, ufugaji, mafunzo ya biashara na kujiajiri sambamba na utoaji mkopo wa fedha taslimu na vitendea kazi.
Bi. Zena emeeleza kuwa vifaa vitolewavyo kwa wanachama kama mkopo ni pamoja na pikipiki, mashine ya juice za miwa, bajaji, viwanja na mashamba.Aidha ameeleza kuwa taasisi hiyo inatoa mafunzo ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na kisasa.
Katika maadhimisho haya ya sabasaba bi. Zena amewaomba vijana na watu wa kada mbalimbali kutumia fursa hii kujisajiri kwa vikundi kuanzia watu 15 hadi 30 na kusajiliwa katika banda lao.

Mkurugenzi wa taasisi ya ujasiriamali ya House of vision bi. Zena Mulokozi akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na fursa za ujasiriamali kwa vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...