Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akimsikiliza Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi. Gaudensia Simwanza, mara baada ya kutembelea banda hilo kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) leo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Joseph Bushweishaija (kushoto) akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati) mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo kwenye viwanja Saba Saba, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka (aliyevaa tai nyekundu)
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akiongea na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) baada ya kuwatembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa suti) akimsikiliza mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alliyekuwa anamuelezea kuhusiana na uhifadhi wa mambo ya kihistoria ya kwenye vitabu kupitia muziki na makala za video alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...