Bi Oliver Njunwa MKuu wa Kitengo cha Mawasiliano Chuo cha Kodi akizungumza na mwandishi wa habari Said Mwishehe katika banda la TRA kwenye maonesho ya biashara ya Sabasaba katika viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_284016" align="aligncenter" width="640"] Rachel Mkundai Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akimkabidhi zawadi mmoja wa wananchi aliyejiunga na mitandao ya kijamii ya TRA ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.


Na Said Mwishehe Blogu ya Jamii 
CHUO cha Kodi (ITA) kimesema kwa sasa kimeanza kupokea maombi ya wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo wa 2018/2019 na kwamba wamekuwa wakielezea program ambazo wanazitoa. 

Pia kimesema wanafunzi wote wenye sifa watume maombi kwa kozi ambazo wanahitaji kusoma na kwamba wanaosoa chuoni hapo na kumaliza wanaweza kufanya kazi mahali popote kwa kuajiriwa au kujiajiri. 

Akizungumza na Michuzi Blog leo katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ambako ndani yake kuna banda la Chuo cha Kodi Mkuu wa Mawasiliano wa chuo hicho Oliver Njunwa amesema wanaombaji watumie maombi kwa njia ya mtandao kupitia www.ita.ac.tz au http://212.71.252.209/ita-oas/

Ametaja kozi ambazo zinatolewa na chuo hicho ni Astashahada ya Forodha na Usimamizi wa kodi na Stashahada ya Forodha na Usimamizi wa Kodi. 

Pia Shahada ya Forodha na Usimamizi wa kodi, Stashahada ya Uzamili wa Usimamizi wa kodi, Cheti Afrika Mashariki cha Uwakala wa Forodha pamoja na Shahada ya Uzamili ya Sheria ya kodi na usimamizi. 

Alipoulizwa ni kitu gani hasa ambacho wanakifanya katika maonesho hayo, amejibu kuwa wanatumia maonesho hayo kwa ajili ya kuzungumza na watanzania kuhusu uwepo wa chuo hicho na faida zake na kubwa ni kuwahamasisha kujiunga na chuo hicho. 

“Chuo cha Kodi ni chuo pekee kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini katika utoaji wa mafunzo ya forodha na kodi. 

“Chuo chetu kinatoa mafunzo kwa wadau mbalimbali na hiyo imetufanya tupokee wanafunzi kutoka nchi nyingi za Afrika,”amesema Njunwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...