Naye Kaimu Mtendaji mkuu wa OSHA Khadija Mwenda aakizungumza jambo na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam jana. 
Naye Kaimu Mtendaji mkuu wa OSHA Khadija Mwenda akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam jana.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, ajira,vijana na watu wenye Ulemavu Jenista Muhagama amewapongeza Wakala wa Usalama mahali pa Kazi(OSHA) kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano kwa kuondoa baadhi ya tozo zilizokuwa kero sehemu ya Kazi.

Akizungumza jana Katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es salaam alisema tozo hizo zilikuwa chagamoto hasa kwa wawekezaji ambao walikuwa wakiingia hapa nchini.

Jenesta alisema uchumi wa viwanda utawezekana ikiwa Taasisi za serikali zinaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali.

"Ikiwa OSHA wameondoa gharama za tozo sehemu za kazi ni wazi uchumi wa viwanda utawezekanika nchini" alisema

Aliongeza kuwa OSHA wanakazi kubwa ya kuhakikisha sehemu ya Kazi zinakuwa salama hasa katika kipindi hiki walichoamua kuondoa tozo.

Hata hivyo alisema uwepo wa OSHA nchini unasaidia wafanyakazi kufanya kazi katika Mazingira yaliosalama.

Naye Kaimu Mtendaji mkuu wa OSHA Khadija Mwenda aliwaomba wadau wasiogope kuja kujisajili kwani ili mfanyakazi aweze kutenda Kazi ni lazima usalama wake ulindwe.

"Msiogope mje kujisajili tumeondoa tozo zote sehemu ya kazi ni lazima sehemu za Kazi kuwe na Mazingira mazuri" alisema Khadija

Aliongeza kwa kuwataka wananchi wote kutembelea katika banda la OSHA kujionea na kujifunza mambo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...