Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) kuhakikisha linabadili mfumo wa mita zinazotumika sasa kuhamia kwenye mfumo wa kieletroniki ambao utawafanya wateja wake walipe kabla ya kutumia hatua ambayo itasaidia katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti upotevu wa mapato. 

Maagizo hayo ameyatoa mapema leo Julai 4, 2018 alipotembelea shirika hilo mara baada ya kuteuliwa mwishoni mwa wiki kuingia kwenye wizara ambapo amesema awali aliwahi kuteuliwa lakini alikaa muda mfupi ambapo aliacha maagizo kadhaa ikiwemo hilo la mita ambalo kwa sasa amewataka walitilie mkazo. 

Amesema kuwa malengo ya wizara yake kuwa ni kuwafikishia wananchi wanyonge huduma ambayo ni muhimu na hivyo amewataka watendaji wa DAWASCO kutoka na kwenda kushughulikia kero za wananchi na kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati. "Nawaomba tufanye kazi kwa uadilifu na kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa kuwapelekea bili zisizoeleweka kabisa maana hizi mita za zamani zinapoteza maji na vile vile fedha ya shirika," 

Amesema Prof. Mbarawa. Aidha ameongeza suala la wafanyakazi kuingia mikataba ya kiutendaji ambayo anaamini endapo itafuatwa itaweza kubadilisha sura ya shirika hilo huku akiigiza bodi ya wakurugenzi kuhakikisha inaongeza wateja kutoka 290,000 waliopo sasa hadi kufikia 850,000 kwa mwaka hatua ambayo itaongeza mapato zaidi ya mara tatu lakini pia amesema suala la upotevu wa maji lipewe kipaumbele ili kudhibiti fedha nyingi zinazopotea kupitia upotevu huo. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja alitoa maelekezo machache wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ofisi za DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akipokelewa ofisi za DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...