Na Frankius Cleophace, Tarime
MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Glorious Luoga ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza na kukamatwa kwa watu ambao wamehusika kutafuna fedha Sh.bilioni 35 ambazo ni za wananchi wa vijiji vitano.
Amevitaja vijiji hivyo ni Kewanja, Genkuru, Kerende, Nyangoto na Nyamwaga.
Akizungumzia fedha hizo Mkuu wa Wilaya amesema zilipaswa kuingia kwenye akaunti za vijiji kutokana na mikataba iliyokuwepo baina ya vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara.
Amesema lakini watu wachache wakafanya hujuma ya kujipatia fedha hizo kinyume cha sheria.Hivyo ametoa siku 14 kwa kikosi hicho kuhakikisha wote watakaotuhumiwa kutokana na sakata hilo kukamatwa mara moja huku mali zao zinazohamishika na zisizohamishika kukamatwa.
"Na wahusika wote kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu na fedha hizo lazima zirudishwe kwa ajili ya kufanya maendeleo ya wananchi."Hizi ni fedha nyingi ambazo zingeleta maendeleo ya wananchi.Nikipita wananitupia lawama kumbe fedha zipo zinaliwa na watu wachache.Siwezi kufumbia macho suala hili," Luoga.
Luoga amesema kampuni hiyo imeanza kujipatiwa fedha hizo baada ya kufoji mikataba na kusababisha kufuta mikataba ya Vijiji hivyo ya mwaka 1995 kufutwana kisha fedha hizo kuanza kulipwa na Mtu binafsi bila wananchi kunufaika .
Aidha ametoa mwito kwa jamii kuishi kwa kufuata sheria na kudaia kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika kuvuruga Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorios Luoga akiongea na Vyomba vya habari katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akionyesha baadhi ya Mikataba ilikuwa ikisainiwa na kampuni ya Keng’anyi Enterprises Limited pamoja na Mikataba ya Vijiji Vitano ukiwemo Mkataba wa Mwaka 1995.
Baadhi ya Watumishi wa serikali wakiwemo watendaji wa kata wakiwa katika kikao hicho cha Mkuu wa wilaya ya Tarime
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...