Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TIMU ya Kagera Sugar 'Wana Nkurukumbi' wamefanya usajili wa wachezaji saba kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikoso chao msimu ujao wa 2018/19.

Katika usjaili huo Kagera wamemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa  Yanga na Majimaji FC msimu uliopita, Jerryson Tegete kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufikia makubaliano kwa ajili ya kuwatumikia Wanankurukumbi.

Katika usajili huo, Kagera wamefanikiwa pia kupata saini ya  aliyekuwa kipa namba moja wa Ndanda FC, Jeremiah Kisubi kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wakata miwa hao wa Kaitaba, Kagera pamoja na nahodha wake Khemedi Khoja anayepiga namba tatu tofauti uwanjani.

Wachezaji wengine ni kiungo mshambuliaji Majid Khamis kutoka Ndanda Fc kwa kuingia nae mkataba wa mwaka mmoja akiwa sambamba na mshambuliaji Omary Mponda naye kutoka Ndanda akiwa amekamilisha uhamisho wake kwa kusaini mwaka mmoja na Kagera pamoja na beki wa kati Amad Waziri kutoka Ndanda FC naye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga ndani ya Kaitaba na Kagera Sugar.

Beki wa kushoto aliyewahi kukipiga Yanga na Mwadui Fc David Luhende  amemwaga wino wa mwaka mmoja kuitumikia Kagera.Usajili huo unakua ni mkubwa kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu zote ikiwa ni kuimarisha kikosi chao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...