Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii

Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imelifungulia gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa na Serikali kutokana na kile kilichodaiwa kuchapisha habari ambazo zipo kinyume na maadili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam leo, Mkurugenzi wa Mwanahalisi Publisher, Saed Kubenea amesema baada ya kufungiwa gazeti la mwanahalisi walikwenda kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.

Amesema kuwa baada kufungua kesi hiyo iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja, mahakama kuu imeona gazeti la mwanahalisi lilifungiwa kimakosa.

Kubenea ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo amesema kuwa kwa mujibu wa hukumu ya mahakama imeoshenya Waziri hakuwa na sheria katika kulifungia gazeti hilo.

Katika kesi hiyo Mwanahalisi ilisimamiwa na Wakili wawili ambao niJeremia Mtobesya akiongozwa na Wakili wa kujitegemea Dkt. Regemeleza Nshallah.

Katika hatua nyengine amebainisha kuwa wanatarajia kwenda mahakamani kwa ajili ya kumdai fidia waziri aliyelifungia gazeti la mwanahalisi.

Mwaka wa jana gazeti Mwanahalisi lilifungiwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na kile kinachodaiwa kuwa na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

katika taarifa yake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abassi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kuwa serikali imechukua uamuzi wa kulifumgia Gazeti hilo kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017, ambapo kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.
Mbunge wa Ubungo na Mmiliki wa Kampuni ya Hali halisi Publisher , Saed Kubenea akizungumza na Waandishi wa habari juu uamuzi uliochokuliwa na Mahakama kwa gazeti la Mwanahalisi.
Waandishi Mbalimbali wa Habari waliohudhuria katika Mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...