Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza wanafunzi na walimu wa Shule ya sekondari Kibaha kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwenye matokeo ya kidato sita mwaka huu yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule alizozitembelea Januari mwaka huu na kuweka mikakati ya kuhamasisha shule hizo zifanye vyema kwenye mitihani ya Kitaifa.

Waziri Jafo amesisitiza kwamba matokeo haya mazuri yanayoanza kujitokeza kwa shule za serikali yametokana na juhudi kubwa ya Rais John Magufuli katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ambapo shule kongwe zote zipo katika hatua mbalimbali ya ukarabati sambamba na maboresho mengine katika sekta ya elimu. 

Jafo amemshukuru Rais Magufuli kwa moyo wake wa kuipambania jamii ya watanzania hadi kufikia mafanikio hayo makubwa yanayoanza kujitokeza hapa nchini. 

Aidha Jafo ameanza mkakati wa kuzifanya shule za serikali hapa nchini kushika nafasi zaidi ya sita katika ya kumi bora kwa matokeo ya kidato cha sita mwakani. Katika kufanikisha mkakati huo, Waziri Jafo ameitisha kikao cha kazi kwa wakuu wa shule pamoja na walimu wa taaluma wa shule za sekondari za vipaji maalum na shule za serikali zilizoingia katika nafasi ya 30 bora katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu ambapo kikao hicho kinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma Agosti 2 mwaka huu.

Awali, kabla ya pongezi hizo,Walimu na wanafunzi wa Kibaha wamekiri wazi kwamba hamasa aliyotoa Waziri Jafo iliwafanya kuwa na uchungu na nguvu ya mapambano katika elimu hadi kufikia mafaniko hayo makubwa waliyoyapata.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akikagua ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari Kibaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...