Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye,
akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu
namna Kituo cha Mafuta (KOJ) kinavyofanya kazi, wakati kamati hiyo
ilipotembelea bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Mafuta (KOJ), Sixtus Karia akifafanua jambo
kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu namna meli
zinavyopakua mafuta katika kituo cha hicho katika bandari ya Dar es
Salaam, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa upanuzi wa bandari
hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi
Kakoso, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA), wakati kamati hiyo ilipofanya ziara bandari ya Dar
es Salaam.
Muonekano wa kazi zikiendelea kwenye mradi wa upanuzi wa gati namba
1 mpaka 7 katika bandari ya Dar es Salaam. Mradi huo unahusisha gati
mpya ya kuhudumia meli za magari.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...