Na Sophia Mtakasimba(TaSUBa)
KANISA la waadiventista Wasabato Tanzania
limeishukuru Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kutoka nafasi
kwa wanamuziki wa kanisa hilo kujifunza Muziki katika taasisi hiyo,kupitia
program maalumu ya Kozi fupi ya Muziki ya mwezi mmoja iliyoanza tarehe 1 Julai na kuhitimishwa leo.
Akizungumza katika ufungaji wa program hiyo
uliofanyika leo katika ukumbi wa TaSUBa
Bagamoyo, Mhazini wa kanisa la wasabato kutoka Jimbo la Kusini mwa Tanzania ,Mchungaji January Athanas
Sigome amesema kuwa kanisa linaishukuru Sana TaSUBa kwa kutoa nafasi kwa Waimbaji ,Viongozi na watunzi wa nyimbo kutoka
makanisa ya Waadventista wasabato,kujifunza Muziki na anaamini wahitimu wataenda
kuwa chachu ya mabadiliko katika makanisa yao.
Aliongeza kuwa kanisa liliamua kushirikiana na
TaSUBa kuendesha program hiyo ili kuwafanya watenda kazi wake wajifunze muziki
na kuweza kurejesha heshima ya ibada kwa Mungu kama ilivyo katika maandiko
matakatifu ,maana katika nyakati za sasa kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa juu
ya namna bora ya kurejesha ibada ya sifa kwa Mungu.
Aidha
Bw.Sigome alisema kuwa kanisa limeichagua taasisi ya sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa)kwa kuwa ndio sehemu pekee yenye wakufunzi wenye weledi wa
kutosha pamoja na vifaa vya kufundishia vya kutosha.
Nae
Leonard Busee ambaye ni mhitimu wa program hiyo amesema kuwa wakiwa TaSUBa
wamejifunza mambo mengi ambayo awali walikuwa hawayajui ikiwemo upigaji wa
vyombo vya muziki,Falsafa ya muziki ,kusoma muziki pamoja na ufundi wa sauti
Nae mtendaji
mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema kuwa ,kozi hiyo maalumu ni miongoni
mwa program mbalimbali ya kimafunzo
ambayo TaSUBa inatoa kwa makundi maalumu kulingana na mahitaji yao.Pia kozi za
muda mrefu za Stashahada na Astashahada
katika fani za mbalimbali
zinaendelea kutolewa na sasa milango ipo wazi kwa wanaohitaji kutuma maombi ya
kujiunga na chuo.
Mhitimu
mwenye umri mdogo kuliko wote , msichana Naomi Yonazi akipotea cheti cha
ushiriki wa program maalumu ya muziki.
Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye
(wa pili kushoto), pamoja na Mhazini wa kanisa la waadventista wasabato Jimbo
la kusini mwa Tanzania Mchuganji January
Atanas Sigome (anayefuata baada ya Dkt.Makoye ), wakiwa katika picha ya pamoja na
wahitimu wa program maalumu ya mafunzo ya muziki .
Wahitimu
wa Programu maalumu ya mafunzo ya muziki wakiimba katika hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Wakufunzi
wa TaSUBa walioendesha program maalumu ya mafunzo ya muziki wakiwa katika
picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Heri Kaare,Rhoda Mitanda,Peter Zengo,Melkiades
Banyanka na John Sagati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...