NA WAMJW-DAR ES SALAAM
KIWANDA
kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza
adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa kuagiza dawa nje ya
Tanzania.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha
dawa hapa nchini leo jijini Dar es salaam.
"Leo
tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa
cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa
nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini", alisema
Waziri Ummy .
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na kujengwa kwa kiwanda hiko
kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya
manunuzi ya dawa kwani mpaka sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda
kununua dawa nje na asilimia 6 ndiyo inannua dawa nchini.
Waziri
Ummy amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kutapelekea kupunguza muda
wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi 9 mpaka miezi 11
kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo
mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania.
"Tunatumia
mda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine
tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa
na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa
na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora" alisema Waziri Ummy.

Picha ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na Masuala ya Afya, ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na masuala ya Afya wakati akiwa katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...