Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mmoja wa Chama cha Wananchi CUF, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, wakikabiliwa na mashtaka mawali likiwamo la kushawishi rushwa ya Sh Milioni 25.
Washtakiwa hao ni Diwani kata ya Segerea, Edwin Kenan Mwakatobe (33) na Diwani wa kata Mchikichini Joseph John Ngowa (45) wote kutoka Chadena na Diwani wa kata ya Mnyamani kupitia CUF, Shukuru Abdallar Dege (42).Wakili wa Takukuru, Devotha Mihayo kutoka Takukuru amewasomea washtakiwa mashtaka yao leo Julai 30.2018 mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Mujaya.
Katika shtaka la kwanza mshtakiwa Mwakatobe anadaiwa tarehe isiyojulikana, Julai 2018 katika Wilaya ya Ilala akiwa Diwani wa kata ya Segerea na mjumbe wa kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alishawishi rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd, Burhan Mvungi kama kichocheo cha kupendelewa katika tenda na LG/015/2017/2018/HQ/CS/07 Lot 03 ambayo nilikuwa chini ya muajiri wao.
Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa madiwani hao, Mwakatobe, Ngowa na Dege Julai 24, 2018 katika baa ya Kwetu Pazuri iliyopo Tabata Wilaya ya Ilala, wote wakiwa wajumbe wa kamati ya fedha na utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walipokea rushwa ya Sh milioni 3 kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd, Burhan Mvungi kama kichocheo cha kupendelewa katika tenda na LG/015/2017/2018/HQ/CS/07 Lot 03 ambayo ilikuwa chini ya muajiri wao.
Hata hivyo, washtakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo wako nje kwa dhamana.Kesi imeahirishwa hadi Agosti 13 , mwaka huu wa ajili ya kutajwa.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika, katika tarehe hiyo washtakiwa hao watasomewa Maelezo ya awali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...