UONGOZI wa Klabu ya KMC Fc imefanikiwa kupata saini ya aliyekuwa mchezaji wa Stand United, Ally Ally na kuitumikia klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Ally Ally amejiunga na KMC FC ya Kinondoni, iliyopanda ligi kuu msimu wa 2018/19 baada ya kumalizana na waajiriwa wake wa zamani.

Beki huyo aliyekuwa mwiba mkali katika mechi za ligi kuu msimu uliopita akiitumikia Stand United amejiunga na KMC baada ya mambo kutoenda sawa katika klabu yake ya zamani kutokana na kutolipwa fedha za mshahara wake.

Ally ambaye ni beki huyo wa kati hivi karibuni aliibuka na kusema Stand kuwa anaidai mshahara wa miezi takribani mitatu na akaadhidi hataweza kuendelea kuichezea klabu hiyo.

KMC ambayo imepanda kushiriki Ligi Kuu Kuu Bara msimu ujao imezidi kukifanyia maboresho kikosi chake ambapo imenyaka saini za wachezaji wenye uzoefu katika ligi ikiwemo kipa Juma Kaseja aliyewahi kung'ara Simba.
 Meneja wa timu ya KMC Fc Walter Harrison(kushoto) akikabidhiana mkataba na beki wa kati Ally Ally baada ya kutia saini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo.
Beki wa kati Ally Ally akitia saini kandarasi ya kuitumikia klabu ya KMC Fc akishuhudiwa na Meneja wa timu hiyo Walter Harrison.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...