Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Mkulima Hassan Sangali (22) mkazi wa Pingalama wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kukamatwa akiwa na vipande Tisa vya meno ya tembo.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Juni 9, 2018 eneo la Kimara Wilaya ya Ubungo mshtakiwa huyo alikamatwa na vipande hivyo Tisa chenye thamani ya dola za marekani 30,000 ambapo ni sawa na Sh 66,720,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 23,2018 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamepeekwa rumande wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...