MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali amezindua rasmi madarasa 2 na mabweni 3 yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Gulamali ameeleza kuwa huo ni moja kati ya miradi ya kimaendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika jimbo hilo na amefurahi kuzindua mradi huo ambao utawasaidia wanafunzi wengi kutimiza ndoto zao kielimu.
Aidha ameeleza kuwa miradi ya kimaendeleo katika sekta ya afya, Umeme, elimu na miundombinu ni muhimu kwa wananchi katika kuleta maendeleo hivyo kama serikali hawana budi kuipa kipaumbele. Katika mwaka huu wa fedha, vijiji vyote katika jimbo la Manonga vitapata umeme na tayari Mbunge huyo ameshatekeleza ahadi yake kwa kukabidhi gari jipya la wagonjwa jimboni humo.
Uzinduzi wa madarasa na mabweni hayo utawasaidia wanafunzi kujiunga na elimu ya kidato cha tano Mkoani humo na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekondari ya juu kutokana na uhaba wa shule.
Katika uzinduzi huo Gulamali aliambatana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka WCB wakiongozwa na Lavalava pamoja na Maromboso walioambatana na jopo la timu yao.
Mradi wa madarasa 2 na mabweni 3 yaliyozinduliwa na mbunge wa Manonga yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...