Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Raia wa Marekani mkazi wa jimbo la Michigan, Lione Lionel Rayford, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kukutwa na zaidi ya kilo mbili dawa za kulevya.

Mmarekani huyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha sheria Namba 15 (1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya sheria Namba 15 ya mwaka 2017. Inayosomeka pamoja na paragrafu 23 ya Jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200 marejeo ya 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 3 ya 2016.

 Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Constantine Kakula amedai kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Julai 4, 2018 huko katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Wanjah Hamza inedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa alikutwa akisafirisha Madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye uzito wa kilogramu 2.188.

Hata Hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Madawa ya kulevya hadi mahakama Kuu au mpaka wapate kibali kutoka kwa DPP.

Kufuatia hayo, mahakama imeamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi Julai 19, 2018. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii ndiyo Raisi Magufuli alikataa kusema kwamba upelelezi hujakamilika wakati mtu kaisha shikwa na madawa na ushahidi upo. Kama serikali inataka kufanya deal na yeye ya kumpunguzia mika kwa kuwasema vigogo waliomuuzia hiyo inaruhusiwa. Mtu kashikwa na dawa upelelezi haujakamilika maana yake nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...