Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,kanda ya Kaskazi.

MAHAKAMA kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi imewahukumu washtakiwa watano kunyongwa hadi kufa ,huku ikimuachia huru mshtakiwa wa pili ambao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite,Bilionea, Erasto Msuya.

Waliohukumia adhabu ya kifo ni mshtakiwa wa kwanza Sharif Athuman ,mshitakiwa wa tatu,Musa Mangu,Mshitakiwa wa tano,Karim Kihundwa,mshitakiwa wa sita ,Sadiq Jabir na mshtakiwa wa saba,Alli Majeshi.

Akisoma hukumu hiyo jana ,Jaji Salma Maghimbi wa Arusha alisema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kwamba washtakiwa watano ndio waliohusika kutekeleza mauaji ya kukusudia ya mfanyabiashara huyo lakini imeshindwa kumtia hatiani mshitakiwa wa pili ,Shaibu Said maarufu Mredii kutokana na ushahidi kushindwa kumuunganisha katika tukio la mauaji.

Awali akisoma maelezo ya kila Mshtakiwa kabla ya kutoa hukumu ,Jaji Maghimbi alisema katika shauri hilo namba 12 la mwaka 2014 upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 27 na vielelezo 26 ambapo vielelezo 21 kati ya hivyo ni vya maandishi na vitano ni ushahidi wa vitu.

Jaji Maghimbi mesema upande wa utetezi uliwasilisha Mashahidi nane pamoja na vielelezo vinne vya maandishi huku akitaja baadhi ya vielelezo vilivyo wasilishwa na upande wa jamhuri kuwa ni pamoja na Pikipiki mbili moja aina ya King Lion namba T751 CKB na Toyo namba T316 CLG zinazotajwa kutumika kutumiwana washtakiwa.

Vielelezo vingine vilivyowasilishwa mahakamani hapo ni pamoja na maelezo ya Onyo ,yaliyotolewa na washtakiwa wa kwanza ,Sharif Athuman, wa tatu ,Musa Mangu na wa saba,Alli Majeshi huku maelezo ya ungamo yakitolewa na Karim Kuhundwa.

Aidha Jaji Maghimbi ameeleza kuwa awali shauri hilo lilikuwa na washitakiwa saba ambapo mmoja kati yao, mshtakiwa wa wanne Jalila Zuberi, Mahakama ilimuachia huru Mei 29,2018 kutokana na kutokupatika na kutotajwa mahala popote wakati wa uwasilishwaji wa ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...