SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limedhamiria kutoa mikopo ya riba nafuu kwa sekta isiyo rasmi wakiwamo wajasiriamali, waendesha bodaboda, mamalishe, wakulima, wavuvi na wote waliojiunga kwenye vikundi rasmi vya uzalishaji mali kama VIBINDO, AMCOS, VICOBA na  SACCOS  

Akizunngumza leo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendeelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ,Kaimu Meneja na Uhusiano wa NSSF Salim Khalfan amewaambia waandishi kuwa NSSF imedhamiria kuinua maisha ya Watanzania kwa kupitia fursa hii ya mikopo ambayo itawawezesha katika kufanya maendeleo yao ya sasa na baadae.

Amesema wafaidika na mikopo hii ni wale ambao wamejiunga tayari kwenye vikundi mbali mbali ambavyo tayari vimesajiliwa na kutambulika vitawezeshwa kuweza kupata mikopo hii kupitia katika benki ya AZANIA.

Hii ni fursa pekee kwa wale ambao wako kwenye sekta isiyorasmi kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya riba nafuu. Shirika la Taifa Hifadhi za jamii (NSSF) linatoa mkopo huo kwa walengwa wenye masharti na fuu na riba ndogo ya kiasi cha asilimia 12.5 ambapo kwa mtu wa kawaida anaweza kukopa na kufanyia maendeleo yoyote.

Pia mbali na wananchi waliopo kwenye sekta isiyo rasmi pia hata wananchi waliopo kwenye sekta iliyorasmi nao wananafasi ya kupata mkopo kupitia vyama vyao vya ushirika. Mbali na mikopo hiyo, wanachama watapata mafao yote sita yanayotolewa na NSSF yakiwemo matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake wanne, mafao ya uzazi ambapo mwanachama mwanamke atapata asilimia 300 ya kipato chake cha mwezi pale mwanachama anapokuwa ameka akiba kwa muda wa miezi 36.

Vile vile mwanachama atapata mafao ya uzeeni pale atakapokuwa amefikisha umri wa miaka 55-60 na mwanachama awe ameshachangia angalau miezi 180. Pamoja na hayo mwanachama atapata mafao ya ulemamu pale itakapothibitika kwamba amepoteza uwezo wake wa kufanya kazi, mafao ya urithi kwa wategemezi wa mwanachama pindi mwanachama atakapofariki pamoja na msaada wa mazishi kwa mwanachama .


Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara alipozungumza nao leo kuhusu dhamira ya Shirika hilo kutoa Mikopo ya Riba nafuu kwa sekta isiyo rasmi kama vile wajasiliamali,waendesha boda boda,Mamalishe,Wakulima,Wavuvi na wote waliojiunga kwenye vikundi rasmi vya uzalishaji mali kama AMCOS,VICOBA  pamoja na SACCOS, ndani ya Banda la Shirika hilo
 katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zitolewazo na shirika hilo mapema leo mbele ya Waaandishi wa Habari (hawapo pichani) wndani ya Banda la Shirika hilo 
katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...