Na.Vero Ignatus Ngorongoro
Mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa elimu sayansi na Teknolojia William Olenasha ameanza ziara ya kutembelea wananchi wa jimbo lake kwa ajili ya kueleza kazi aliyofanya kwa muda wa miaka mitatu tangu achaguliwe na wananchi wake ikiwemo mradi wa barabara ya Lami kutoka Loliondo mpaka Mto wa Mbu.
Imekuwa ni desturi ya mara kwa mara kwa mbunge huyo kutembelea wananchi wake kila kata ambapo kila kata amepita mara nne tangu achaguliwe kuwa muwakilishi wa wananchi Bungeni.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ngaresero pamoja na kata ya Pinyinyi zilizopo katika wilaya hiyo Olenasha amesema kuwa yeye ni mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi wanyonge ambao wana changamoto hivyo lazima azitatue kwa kuwa ndiyo jambo alilotumwa na wananchi kuwawakilisha.Amesema kwasasa serikali inayoongozwa na Raisi John Magufuli imejitofautisha sana na kipindi cha nyuma kwakuwa hata maeneo ambayo yalisahaulika kwa muda mrefu kwa sasa yameshaanza kupatiwa vipau mbele ikiwemo pia miradi mikubwa ambayo imepelekwa katika jimbo hilo la Ngorongoro.
Olenasha amesema kuwa tayari kupitia yeye kama mbunge wananchi wameshaanza kuletewa mradi mkubwa wa barabara ya lami ambao ni wa kihistoria kutoka Loliondo mpaka mto wa Mmbu kilomita 213 mradi ambao wengi walizani ni ndoto tayari umeshaanza kujengwa.“Napenda kuwataarifu wananchi kuwa ujenzi wa barabara ya lami umeshaanza na shilingi Bilioni 87 zimeshatolewa tayari jambo ambalo wengi walidhani ni ndoto lakini imewezekana na mradi umeanza kwa ksi kubwa”Alisema Olenasha
Hata hivyo Olenasha amemshukuru Raisi Dokta Magufuli kwa kuwapa kipau mbele katika kuletea wananchi wake maendeleo ambapo nje na mradi huo wa Barabara upo mradi wa Umeme,Afya,maji na Elimu ambapo miradi hiyo imeshaidhinishiwa fedha kwa ajili ya kuanza mara moja.Kwa upande wa wananchi ambao wameshiriki mkutano huo wa Mbunge wamesema kuwa tangu kuanza kwa historia ya Uhuru hawajawahi kupata mawasiliano hata ya Simu wala kuona kituo cha afya lakini kupitia mbunge wao wameona mafanikio hayo.
Pamoja na hayo wamesema kuwa mbunge wao amekuwa mstari wa mbele katika suala la maendeleo kwasababu kila mara anatembea jimboni kwake licha ya kuwa na changamoto zilizopo lakini wanampa ushirikiano mzuri ili afanikishe kile ambacho ameshakianza kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Olenasha,ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ngorongoro William Olenasha akizungumza na wananchi wa jimbo hilo.
Wananchi wa kijiji cha Ngarasero wakimsikiliza mbunge wao Wiliam Olenasha katika ziara yake ya kutembelea wananchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...