Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KAMANDA
wa Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kufariki dunia kwa watu watano
baada ya kutokea ajali ya kugongana magari matatu jana usiku na
kinachoendelea asubuhi ya leo ni kuiondoa miili ya watu wawili ambayo
imeng'ang'ania katika gari.
Ajali hiyo imetokea jana usiku katika eneo la Mlima Igawilo nje kigogo ya Mji wa Mbeya Mjini na kusababisha video vya watu hao.
Akizungumza
na Michuzi Blog kwa njia ya simu asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Urich Matei amesema katika ajali hiyo wote waliofariki ni wanaume na kwamba
watu watatu walifanikiwa ukitoa miili yao eneo la ajali na kuipeleka
chumba cha kuhifadhia maiti.
"Kwa
sasa asubuh hii tupo eneo ambao ajali imetokea kwani kuna miili ya watu
wawili bado tunahangaika kuitoa katika gari. Imekandamizwa ndani ya
gari ndogo aina ya Noah ambayo ililaliwa na kontena.
"Hivyo
tunaendelea kuitoa miili ya watu hawa.Idadi ya watu waliokufa ni watano
na majeruhi mtu mmoja. Chanzo cha ajali imetokana na lori ambalo
limebeba kontena kufeli breki na kusababisha gea boksi kukatika na hivyo
kupoteza muelekeo,"amesema Kamanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...