Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

SHIRIKA la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na Benki za Azania,NMB na NBC  kwa  ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanachama wake watakao ingia kwenye mpango wa Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, lengo likiwa ni kupunguza hali ya umaskini.

NSSF  imeanza utekelezaji wa mpango huu baada ya maboresho ya sheria namba 2 ya mwaka 2018 iliyotoa majukumu kwa shirika hilo kuboresha na kushuhulikia sekta isiyo rasmi ambayo inatajwa kuwa kwa muda mrefu imetelekezwa.
Katika kuhakikisha elimu hii ya inawafikia wananchi wengi ,NSSF imeanza kufanya mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya wajasiriamali ili kutoa hamasa na baadae kuwaingiza katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wananchi wote ambao wako kwenye sekta isyo rasmi.
Mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Moshi,Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Kippi Warioba akatumia nafasi hiyo kutoa rai kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya ubadhirifu.
Kwa upande wao washiriki wa Semina hiyo wakiwemo viongozi wa Benki zilizoingia mkataba na NSSF katika kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanachama walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo wajasiliamali wadogowadogo wameelezea matumani yao juu ya mpango huo wa NSSF.
Wanachama ambao watanufaika na mpango huu ni wale watakao toka kwenye vikundi vyenye sifa za mikopo ambayo itasimamiwa na Benki ya Azania zikiwemo Saccos na Amcos zaidi ya 100.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizunguza wakati wa Mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF)  kwa Wajasiliamali ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaingiza wote walio kwenye sekta isiyo rasmi katika Mifuko ya Jamaa .

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibisha Sera wa Shirika la Mifuko ya Jamii,(NSSF) Mariam Muhaji akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwemo wawakilishi wa Benki za Azania na NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...