Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema wameyapokea maoni ya wadau na watayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utoaji na urejeshaji wa mikopo.
Badru aliyasema hayo wakati akizungumza katika banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kwenye maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Amesema kuwa HESLB inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wazazi, wanafunzi pamoja wanufaika wa mikopo.
Amesema kuwa wadau wakifika katika banda la bodi watapata ufafanuzi wa vipengele kwa waombaji mikopo katika bodi hiyo utakaomalizika Julai 15 mwaka huu kwa waombaji hao kupata taarifa sahihi.
Badru amesema kuwa wanufaika wa mikopo pia watapata elimu ya urejeshaji wa mikopo iliyoiva ili kuweza kurejesha katika mfuko kwa ajili wengine kunufaika ikiwa ni pamoja na kujua ankara zao kwa ajili ya kulipa kutokana na kuwepo na changamoto katika malipo.
Badru amesema kuwa wanufaika wa mikopo pia watapata elimu ya urejeshaji wa mikopo iliyoiva ili kuweza kurejesha katika mfuko kwa ajili wengine kunufaika ikiwa ni pamoja na kujua ankara zao kwa ajili ya kulipa kutokana na kuwepo na changamoto katika malipo.
Aidha amesema kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa na mwamko wa kukata asilimia 15 ya mshahara huku wengine wakikata bila kupeleka bodi kwa wakati muafaka.Amesema waajiri ambao wamekuwa wakishindwa kufanya malipo kwa wafanyakazi wao wamekuwa wakiwapeleka mahakamani na wakifika huko wanaomba wazungumze nje ya mahakama na matokeo yake wanalipa.
01.Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Blog katika banda la bodi hiyo katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akiwapa huduma wananchi waliotembelea banda la bodi katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Prof. Joe Lugalla akipata maelezo katika banda la bodi ya mikopo alipotembelea maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...