Na Frankius Cleophace Serengeti
SHIRIKA la Righ to Play linaendelea na matamasha katika kata za wilayani Serengeti mkoani Mara kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na masuala ya ukatili wa ijinsia dhidi ya watoto.
Elimu hiyo inayotolewa inazungumzia kupiga vita ukeketaji kwa mtoto wa Kike, mimba za utotoni, vipigo kwa watoto, kuchomwa moto pamoja na kuhakikisha wanapata haki ya elimu bila kubagua jinsia.
Akizungumzia kuhusu tamasha lililofanyika kata ya Uwanja wa Ndege, Leah Kimaro kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY amesema lengo la Shirika ni kuhakikisha wanabadili mitazamo ya jamii ili kuondokana na mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati ili kumkomboa mtoto wa kike ambaye kwa Serengeti amekuwa akiachwa nyuma kutokana na mila hizo.
Ofisa Maendeleo Jamii Kata ya Uwanja wa Ndege Josepha Dismas ameitaka jamii kuendelea kuthamini watoto wote bila ubaguzi wowote na kuahidi kuwa wao kama Serikali wataendelea kushirikiana na mashirika ili kuipatia jamii elimu iliyokusudiwa.
“Hii elimu inayotolewa kupitia michezo mbalimbali ukiwemo mpira wa miguu kwa wasichana jamii inazidi kuamini kuwa Mtoto wa kike anaweza bila kuwezeshwa."Hivyo sasa ni jukumu letu kama viongozi ngazi za jamii kushiriki kikamilifu na kuzidi kulaani Vikali ukatili unaofanyika kwa Watoto,” amesema Josepha.
Pia Ofisa Maendeleo ameongeza kuwa michezo hiyo imezidi kukusanya watoto wengi na maudhurio kuongezeka mashuleni,hivyo wazazi wameombwa kuruhusu watoto wao ili washiriki michezo.

Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uwanja wa Ndege Josepha Dismas akikabidhi Kapteni wa Timu ya Senta FC baada ya kushinda Timu ya Burunga FC.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uwanja wa Ndege Josepha Dismas akikabidho Kombe kapteni wa Timu ya Vilaza Fc baada ya kushinda Timu ya Vibonde FC.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Uwanja wa Ndege Josepha Dismas akikabidhi Zawadi ya Madaftari kwa Wanafunzi hao walioshiriki Vyema katika Michezo iliyofanyika Maeneo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...