Na khadija seif ,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 420 na Benki ya KCB kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu Benki ya KCB nchini Cosmas Kimario ameeleza madhumuni ya Benki hiyo ni kushirikiana na TFF kwa ajili ya kukuza sekta ya Michezo, ambapo hapo awali walishirikiana kwenye msimu uliopita 2017/2018 kwa kuwa moja wa wadhamini wa ligi kuu nchini.
Kimario amesema udhamini huo unalenga zaidi kuendeleza soka hilo nchini pamoja na kuwapatia ajira vijana na kuipeperusha bendera ya nchi ya Tanzania.
Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Wallace Karia ametoa shukrani za dhati kwa benki ya KCB kwa udhamini huo, kwani watanufaika na kusaidia kunyanyua michezo katika msimu wa 2018/19. Hata hivyo Karia amesema Benki ya KCB imekuwa ikishirikiana na TFF kwenye michezo na hata msimu uliopita walishirikiana nao kudhamini michezo nchini na hii ikiwa ni mara ya pili.
Kaimu mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Fatma Chiro ameeleza Benki hiyo imetoa ajira kwa watu wengi na rasmi,hivyo inaunga mkono kauli ya serikali katika kutoa ajira kwa vijana na wameamua kuanza na sekta ya michezo.
Amefafanua zaidi kuwa benki hiyo haitaishia hapo kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu (TFF) katika kudhamini michezo hususani mpira wa miguu na kutazama uwezekano wa kusaidia timu ya mpira wa miguu ya wanawake Kilimanjaro Queens ambao wameshinda mechi waliocheza hivi karibuni dhidi ya Ethiopia na kurudi na kombe nchini Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace
Karia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420
kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chilo baada ya
kusaini mkataba wa udhamini kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas
Kimario na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface
Wambura.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...