Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UCHAGUZI wa kihistoria bila kuwepo kwa jina la aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kama mgombea umefanyika leo nchini Zimbabwe.
Imeelezwa kuwa zaidi ya watu milioni 5 wamejiandikisha na kujitokeza kupiga kura wakiwa na shauku ya kuona mabadiliko baada ya utawala mrefu wa Robert Mugabe(94).
Wagombea wanaochuana vikali ni Rais Emmerson Mnangagwa (75) kutoka ZANU-PF aliyekaimu nafasi mara baada ya Mugabe kujiuzulu na mwanasheria Nelson Chamisa (40) kutoka MDC.
Robert Mugabe amenukuliwa akisema kuwa uchaguzi huu utaiondoa serikali isiyo ya kikatiba madarakani, kauli hii imetafsiriwa kuwa Mugabe anaunga mkono upinzani licha ya Chamisa kukanusha hivyo.Chamisa amejihakikishia ushindi mara baada ya kupiga kura.
Mwaka 1987 Mugabe alichukua kiti cha urais na kuhudumu kwa miaka 37 hadi November 2018 ambapo jeshi la nchi lilipompindua na makamu wake kukaimu nafasi hiyo na hii ni baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu huyo kazi kwa kuamini utawala wa Mnangagwa ni haramu na fedheha kwa nchi yao.
Rais Mstaafu wa Zimbabwe Robert Mugabe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...