NAIBU Katibu wa Wizara ya Fedha na Mipango Suzana Mkapa amesema kuwa Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) ni iendelee kusimamia taaluma katika kuandaa vijana watakaotumika kwa tija.


Naibu Katibu Mkuu huyo aliyasema hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika maonesho ya 42 ya Biashara Kimataifa katika viwanja Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam amesema kuwa serikali inakwenda katika uchumi wa viwanda hivyo wahasibu wataozalishwa watakweda katika viwanda.

Amesema kuwa maonesho ni sehemu ya kujitangaza hivyo watumie fursa ya kuwahudumia wananchi wanaopita katika banda hilo kwani wakati mwingine baadhi wanakosa taarifaza chuo.

Ameongeza kuwa serikali kazi yake ni kuona kila chuo kinazalisha watalaam wengi ambao watazalisha na kuliletea taifa maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Suzana Mkapa akizungumza katika banda la Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) katika maonesho ya 42 yaBiashara Kimataifa katika viwanja Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Suzana Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa TIA wanaotoa huduma katika maonesho ya 42 yaBiashara Kimataifa katika viwanja Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...