UONGOZI wa Yanga umemtambulisha kiungo mahiri Mohamed Banka aliyekuwa anakipiga katika kikosi cha Mtibwa Sugar.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga Hussein Nyika amesema kuwa Banka amesaini kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kutumikia kikosi cha wana jangwani hao.

Amesema kuwa, wamemsajili Banka kwa mapendekezo ya kocha kwani aliweza kumfuatilia kipindi cha ligi kuu.

Kwa upande wa Banka mwenyewe amesema kuwa amekuja Yanga kucheza mpira na kuirjesha Yanga katika viwango vyake.

Banka amesema anajua kuwa kuna ushindani wa namba hasa kwa timu kubwa kama Yanga ila kikubwa ni mazoezi tu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga Hussein Nyika akiwa pamoja na Kiungo Mohamed Banka baada ya kutambulishwa pembeni ni Meneja wa timu Hafidh Saleh.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...