Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (Trade and Development Bank-TDB), itaikopesha Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 400, sawa na takriban shilingi bilioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) na Mradi wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kilwa.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Rais wa Benki hiyo yenye Makao yake Makuu Jijini Nairobi Nchini Kenya, Bw. Admassu Tadesse, alipokutana na kufanya mazungunzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.

Bw. Tadesse amesema kuwa Benki yake imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati ya kisasa pamoja na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kilwa mkoani Lindi.

"Tanzania ni mdau mkubwa wa Benki hii ikiwa inashika nafasi ya 7 kati ya nchi na taasisi 37 zinazomiliki hisa zake ambapo inamiliki hisa asilimia 6.4" alisema Bw. Tadesse.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akijadiliana na ugeni wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika - TDB (hawamo pichani) kuhusu uboreshaji wa sekta ya nishati ya umeme ili kujenga uchumi wa viwanda.  Kulia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo.
 Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB, Bw. Admassu Tadesse (katikati) akitoa ufafanuzi wa mkopo wenye masharti nafuu utakaosaidia ujenzi wa Reli ya Kati ya Kiwango cha Kimataifa(SGR) na nishati ya umeme pamoja na miradi mingine midogomidogo. Kulia ni Mkuu wa Wakala wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB Bi. Neema Siwingwa na kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Kisheria wa Benki hiyo Bw. David Bamlango.
 Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (kulia) ukijadiliani na ujumbe wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB (kushoto) namna ya kufadhili ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa -(SGR) na Mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya Gesi wa Kilwa.
  Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (kulia) ukijadiliani na ujumbe wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB kwenye picha ya pamoja mara baada ya majadiliano ya namna Benki hiyo itakavyoikopesha Serikali kiasi cha dola milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa pamoja na Ujenzi wa mradi wa Umeme wa Gesi wa Kilwa utakaozalisha megawati 318 za umeme.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...