*Utafanyika kuanzia Julai 17 hadi Julai 18 mwaka huu, Rais Magufuli kutoa neno

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
UKWELI ni kwamba macho na masikio ya nchi mbalimbali barani Afrika na nchi nyingine duniani yatajikita nchini Tanzania kuanzia Julai 17 hadi 18 mwaka huu.

Unajua kwa nini?Ni kwasababu kutafanyika mkutano wa vyama vya siasa wenye hadhi ya dunia na Tanzania imepata nafasi ya kuandaa mkutano huo ambao umeratibiwa na Chama cha Kikomunisti cha China(CPC).

Ni mkutano unaolenga kujadili mambo mbalimbali na hasa mchango wa vyama vya ukombozi barani Afrika sasa kuweka mikakati ya kujenga uchumi imara kwa nchi za Afrika.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole ni akizungumzia ujio wa mkutano huo amesema utahudhuria na na zaidi ya watu 138 kutoka nchi mbalimbali zikiwamo za nje ya Bara la Afrika na vyama zaidi ya 30 vitashiriki.

Kwa mujibu wa Polepole waadau mbalimbali wakiwamo viongozi mashuhuri, wanasiasa wakongwe na watu maarufu watashiriki na kutoa mchango wao kwa maslahi ya vyama hivyo na Bara la Afrika kwa ujumla.

"Tanzania inatarajia kupokea ugeni mkubwa wa viongozi ambao watakuja kushiriki kwenye mkutano huo wa kidunia,"amesema Polepole wakati anazungumzia mkutano huo.

Kwanini mkutano huo unafanyika Tanzania? Majibu yanaweza kuwa mengi kulingana na mhusika atakavyoona inafaa.

Lakini ukweli ni kwamba mkutano huo unafanyika nchini kutokana na utulivu, amani , upendo na mshikamano na kubwa zaidi ni urafiki wa kidugu na wa damu wa muda mrefu kati yetu na nchi ya China.

Kwa kukumbusha tu kabla ya mkutano huo kuamriwa kufanyika Tanzania kuna nchi nyingi nazo zilitamani mkutano huo ufanyike kwenye nchi zao na moja ya nchi hizo ni Afrika Kusini.

Baada ya CPC kupima na kuchuja wakaona eneo ambalo ni sahihi kuufanyika mkutano huo ni Tanzania na ikumbwe ni mkutano wa kwanza mkubwa wa China kufanyika nje ya nchi yao.
Nieleze japo kidogo umahiri, uhodari na uchapa kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli umechangia kwa kiasi kikubwa China kuamua mkutano huo ufanyike nchini.

Hivyo kabla ya kuendelea nitumie fursa hii kutoa pongezi na shukrani kwa Rais Magufuli kwa utendaji kazi wake ambao umewakuwa ukiwafurahisha mataifa makubwa mbalimbali duniani likiwamo Taifa la China.

Pamoja na yote iko hivi nia ya CPC ya kuhakikisha kunafanyika mkutano huo ni kuangalia namna ambavyo watajadiliana na viongozi wa vyama vya ukombozi katika kusukuma maendeleo ya Afrika mbele.

Kwa Tanzania ni fahari kubwa mkutano huo kufanyika nchini kwetu kwani pamoja na mambo mengine itakuwa fursa ya kujifunza na kupata uzoefu wa mambo mbalimbali yakiwamo ya teknolojia na  uchumi.

China kupitia viongozi wake mahiri na wenye kuheshimika duniani ambao wanatokana na CPC wamekuwa mfano wa kuigwa katika maendeleo ya kukua kiuchimi na kulifanya Taifa hilo ndani ya miaka 73 limepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...