Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla kipengele cha (Trade in Services Exhibitor) Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Ltd Masoud Khalfan Saeed jana. Mara baada ya kutangazwa washindi katika uzinduzi wa maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya TANTREADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Property International Ltd Masoud Khalfan Saeed akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha Redio cha Uhuru FM wakati walipotembelea katika banda hilo.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda hilo.
Baadhi ya wateja wakipata huduma mbalimbali za kununua viwanja.
Baadhi ya wananchi wakiangalia maeneo yenye viwanja katika ramani.

Said Mwishehe Blogu ya Jamii
PROPERTY International Ltd baada ya kupata ushindi katika eneo la Trade in Services Exhibitor limewahakikishia Watanzania kuendelea kutoa huduma bora huku wakijivunia kuwa wamejipanga vema.

Kauli hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwakabidhi kikombe cha ushindi katika eneo hilo wakati anafungua Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Kwa kukumbusha tu Property International Ltd ambayo imejikita katika uuzaji wa viwanja ambavyo vimepimwa kitaalam , vinapitika na barabara zimechongwa , huduma za maji na umeme zipo karibu.

Akizungumzia ushindi ambao wameupata Mkurugenzi wa Property International Ltd Masoud Khalfan Saeed amesema ushindi huo umedhihirisha namna ambayo wamejipanga katika kuwahumia wananchi.

“Tumefurahi kushinda katika eneo hilo la Trade in Services Exhibitor na ni uthibitisho tosha kuwa tulijipanga vya kutosha.Kikubwa ambacho tunaahidi ni kuendelea kutekeza majukumu yetu katika kiwango cha juu cha utoaji huduma,”amesema Saeed.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...