Na Agness Francis, Globu ya Jamii

WANAYANGA wamechukizwa na kitendo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Yanga Abbasi Tarimba kuzungumza habari za klabu hiyo zisizokuwa na uhakika kwenye kituo cha redio.

Wamedai kuwa Mwenyekiti  huyo ameongozana mpinga maendeleo wa Yanga Mohammedi Msumi kwenda redioni,ikiwa walichotegemea  kutoka kwake ni kuelezea ameifanyia nini klabu hiyo toka alivyochaguliwa Juni 10 mpaka leo Julai 10 mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es  Salaam  Mwenyekiti wa  matawi ya klabu ya yanga Tanzania Bakili  Makele amesema  kuwa fedha za Sportpesa  zinatoka kwa mujibu wa mikataba na si kwa matakwa ya Tarimba kama anavyojinasibu kuwa amelipa wachezaji,ikiwa hakuna fedha yake yoyote  iliyopokelewa klabuni.
Makele amekanusha kuwa hakukuwa na taarifa ya kuvunjwa  kwa kamati hiyo ya Tarimba katika mkutano wao uliofanyika,ingawa  wanachama hao walileta hoja hiyo mezani
Makele amesema katika hoja hiyo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga alikataa na kwa kuwa hakuwa na majukumu ya  kuvunja mamlaka ya mkutano mkuu.
"Tunasikitika kwa hesmima ya Tarimba  hapaswi kukurupuka kama anavyopokea taarifa kwa akina msumi na kuzifanyia maamuzi,sasa tunaamini adui mwingine wa maendeleo ya klabu ya yanga ni yeye,amesema Makele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...