Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amemwaga Sifa kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa jitiada binafsi za kuwaboreshea Walimu mazingira ya kazi ikiwemo ujenzi wa ofisi 402 za walimu.Waziri Jaffo ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Pikipiki 2,894 zenye thamani ya zaidi ya shilling Billion 8.5 zilizotolewa kwa waratibu wa elimu Kata ambapo kitaifa Zoezi hilo limefanyika Dar es salaam.
RC Makonda amesema anajivunia kuona Dar es salaam inaendelea kushika kidedea kwenye matokeo ya mitihani ya kitafa kutokana na walimu kuwekewa mazingira bora ya kazi ikiwemo ujenzi wa ofisi 402 za kisasa za walimu, mikopo ya viwanja vya bei nafuu pamoja na kusafiri Bure kwenye daladala na Treni ambapo amesema bado ipo mipango mingi ya kuhakikisha walimu wake wanaishi vizuri ili wawe na motisha ya kazi.
Aidha RC Makonda amesema pikipiki zilizotolewa zitaenda kuongeza nguvu na hari ya kazi kwa waratibu wa elimu Kata ambapo kwa mkoa wa Dar es salaam umepata pikipiki kwa kila Kata.


Kazi nzuri kwa Serikali huo ndio uzalendo halisi. Nmapongeza Mheshimiwa Rais Kwa kuwajali walimu. Si kila mtu atamkubali kwa kazi anayofanya ila ipo siku watasema wamemkumbuka. Ni kawaida ya watanzania japo penye ukweli lazima tuseme. Rais amejenga historia mpya na hili liwekwe kwenye rekodi muhimu kabisa.
ReplyDeleteWaziri Seleman Jaffo tunaiona kazi yako kama waziriwa TAMISEMI.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda kazi yako ni kubwa sana na umekuwa chachu kwa Wakuu wa Mikoa wengine kuiga utendaji kazi wako.
Nawasilisha.