WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu.
Marehemu Ngonyani ambaye alifariki dunia Julai 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi ameagwa Jumatano Julai 4, 2018 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanafamilia, wabunge, wananchi wa Korogwe pamoja na Watanzania kwa ujumla. 
Amewataka waendelee kumuombea marehemu. 
 “Natoa pole kwa wake wa marehemu, watoto na nawaomba tuendelee kuwa wavumilivu na watulivu katika kipindi hiki. Tulimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,”
Kwa upande wake, Katibu wa Bunge, Bw, Stephen Kagaigai akisoma wasifu wa marehemu amesema Bw. Ngonyani alizaliwa Mei 25, 1956 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Bw. Kagaigai amesema marehemu alianza kuugua Juni 17 mwaka huu na Juni 18 alilazwa katika Hopitali ya Mkoa wa Dodoma na Juni 20 alihamishiwa katika Hopitali ya Muhimbili.Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Wabunge na wanafamilia na wananchi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijijini Dar es salam, Julai 4, 2018. 
Wapambe wa Bunge wakiwa wameubeba mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stehen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia wakati alipowaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) wakati alipoongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye viwanja vya Karaimjee jijini Dodoma Julai 4, 2018. Wapili kulia ni Spika wa Bunge Job, Ndugai na wapili kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...