WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kununua madeni yaliyosababishwa na mikopo ya kibenki kwenye vyama vikuu vya ushirika nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.
“Serikali ya awamu ya tano hatuna biashara ya kununua madeni ya vyama vikuu, kulikuwa na tabia ya watu wa ushirika kukopa na hali ikiwa mbaya wanakimbilia Serikalini. Serikali hii hatuna biashara hiyo,” amesema.
Waziri Mkuu amesema anazo taarifa kwamba Chama Kikuu cha mkoa wa Kagera (KCU) kimekopa fedha Benki ili kiweze kulipa deni la mwaka 2014. “Nimeambiwa KCU wamekopa fedha benki ili kulipa deni la mwaka 2014, hii inaingia akilini kweli? Mnakopa fedha kulipa deni la zamani, ni kwa nini msiwatafute waliosababisha deni na kuwachukulia hatua?,” alihoji.
“Ninyi mlikuwa watu sita ambao mlikubaliana kama viongozi, mlienda kukopa kuzidi uwezo mlionao. Leo hii ni kwa nini serikali ije kulipa wakati mmetumia ninyi?,” aliuliza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya tatno inasisitiza masuala ya ushirika kwa sababu imeamua kuwahudumia wananchi kuanzia ngazi ya chini kuanzia pembejeo, dawa hadi masoko.
“Tunataka tuondoe utaratibu wa chama kikuu kukopa fedha benki ili kikanunue mazao. Vyama vingi vimetengeneza hasara, leo hii vyama vikuu vina madeni. Hii ni kwa sababu mlikopa fedha benki wakati hata hamjui mna kilo ngapi ambazo zimevunwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majalawa akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya
ushirika dunianiyaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini
Mwanza, Julai 7, 2018.
Waziri
wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumza wakati alipomkaribisha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia katika Maadhimisho ya siku ya
Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha
jijini Mwanza, Julai 7, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la
Ushirika nchini, Bibi Renata Mwageni (kushoto) Tuzo ya Rais John Pombe
Magufuli iliyotolewa na Wanaushirika nchini ili kutambua mchango wa
Rais katika kuendeleza sekta ya ushirika na kuinua uchumi wa wananchi
wa Tanzani ya 2018 . Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa
Furahisha jijini Mwanza Juni 7, 2018. Wapili kushotoi ni Waziri wa
Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na
na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika
duniani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia
kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mizani ya Kielektroniki ya kupima uzito
wa pamba wakati alipotembelea banda la Chama Kikuu cha Ushirika cha
Nyanza katika maonyesho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika
kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Wapili
kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na watatu kulia ni Naibu
Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwaanjelwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba iliyostawi vizuri wakati
alipotembelea banda la Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza baada ya
kuhutubia katika maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika
kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Kushoto
ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama samaki waliokaushwa wakati
alipotembelea banda la Vyma vya Ushirika katika Soko la Kimataifa la
Kirumba – Mwaloni wilayani Ilemela baada ya kuhutubia katika Maadhimisho
ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa
Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Zainab Telack na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela
.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa TANESCO wakati
alipotembelea banda lao katika maonyesho ya siku ya Ushirika duniani
yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa furahisha jijini Mwanza Julai 7,
2018. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo,
Dkt. Mary Mwanjelwa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...