*Ni baada ya kuchelewesha kukamilisha mradi uliotakiwa kumalizika mwaka 2017

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amemuagiza mkandarasi anayejenga matanki ya kuhifadhia maji na pampu na kusukumia maji kukamilisha mradi huo haraka hadi ifikapo mwishoni mwa Septemba mwaka huu

Amesema mkandarasi huyo Jain Irrigation system kutoka India  hadi sasa amekamilisha asilimia 87. 5 ya mradi huo ulioanza Machi mwaka 2016 na ulipaswa kukamilika Novemba mwaka 2017.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya  kukagua  miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)  ambayo bado ipo kwenye utekelezaji katika maeneo mbalimbali jijini.

 Amesema mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji jijini ni wa muhimu na utagarimu Sh. bilioni 72.43 lakini inasikitisha mpaka sasa bado hajakamilisha.

 "Mradi huu ni muhimu sana kwani watanzania wengi hasa wananaoishi hapa jijini Dar es Salaam wanachangamoto kubwa ya maji,"amesema Mbarawa.

Amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa mradi huo ilikuwa ni kuhakikisha changamoto za maji kwa watanzania  zinakwisha lakini mkandarasi bado analeta shida.

Kutokana na  mapungufu hayo ya Mkandarasi, Waziri Mbarawa amemuagiza Meneja mradi huo, Anil Vitankar kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa haraka na pia amemuagiza mkandarasi huyo kuwepo kwenye eneo la mradi kwa saa 24, na kama akishindwa kumaliza mradi huo kwa wakati waliokubaliana ambao ni mwisho mwezi September basi hiyo ndio itakuwa mara yako ya mwisho kwa mkandarasi huyo kufanya kazi nchini.
  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa (wa pili kulia), akikagua sehemu ya kuhifadhi vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya maji Dar es Salaam na Pwani,  unaosimamiwa na Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa, akitoka kukagua tenki la kuhifazia maji, Mabwepande, Dar es Salaam.
  Profesa Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kumpa maagizo mkandarasi wa Kampuni ya Jain Irrigation System kutoka nchini India  mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya maji Dar es Salaam na Pwani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...