Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Waathirika wa dawa za kulevya wanaoishi katika nyumba ya kurekebisha tabia (Soba House) ya Detroit iliyoko Kwamchina mwanzo wameiomba Serikali kuendeleza mapambano ya kupiga vita uingizaji na utumiaji wa dawa hizo nchini.

Vijana hao walitoa ombi hilo baada ya kupokea msaada wa chakula uliotolewa na Mtandao wa Kijamii Zanzibar 24 ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya kutimia miaka mitatu tokea kuanzishwa mtandao huo.

Kijana Alawi Abdalla anaeishi nyumba hiyo alisema ikiwa Serikali haitaongeza nguvu za kuwatafuta na kuwakamata waingizaji wakubwa wa dawa za kulevya vijana wengi wataendelea kuathirika.

Aliwashauri vijana ambao bado hawajaanza kutumia dawa za kulevya wasijaribu kuzionja  kwani sio kitu cha kuonja na nihatari kwa usalama wa afya zao.

Alawi aliishauri Serikali kuwatafutia msaada wa nyenzo za kufanyia kazi vijana waliopita Soba House na kufanikiwa kurekebisha tabia zao ili watakapo rejea katika jamii waweze kujitegemea.
 Mtendaji Mkuu wa Zanzibar 24 Suleiman Juma Is-haka akimkabidhi Mkuu wa Soba House ya Detroit Rashid Kassim msaada wa chakula katika hafla iliyofanyika katika nyumba hiyo iliyopo Kwamchina mwanzo.
 Baadhi ya vijana wanaoishi nyumba ya kurekebisha tabia ya Detroit iliopo kwa Mchina mwanzo wakifuatilia kukabidhiwa msaada wa chakula uliotolewa na Mtandao wa Kijamii wa Zanzibar 24.
 Mkuu wa Soba House ya Detroit  Rashid Kassim akitoa shukrani zake mbele ya waandishi wa habari wa Zanzibar 24 baada ya kupokea msaada wa chakula katika hafla iliyofanyika kwenye nyumba hiyo Kwamchina mwanzao.
Mmoja wa vijana wanaoishi nyumba ya kurekebisha tabia ya Detroit Alawi Abdalla akizungumza na waandishi wa habari  wa Zanzibar 24 Amina Omar (kulia) na Fat-hiya Shehe katika hafla iliyofanyika Kwamchina mwanzao. Picha na Ramadhani Ali  Maelezo Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...