Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
WATU wawili wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya Basi la Modern Coach lililokuwa likitokea nchini Kenya kuja Dar es salaam kupata ajali katika eneo la Mbwewe, mkoani Pwani.
Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bw. Aminiel Aligaeshi amethibitisha kupokea majeruhi hao leo saa 12 asubuhi.
Akizungumza na Michuzi Blog Aligaeshi amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti na majeruhi wote 10 ambao wamewapokea wanaendelea vizuri. Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba gari iliyopata ajali jali basi hilo lilikuwa na abiria 45, dereva mmoja na tingo mmoja na abiria 43.

Wakati huo huo basi la Maning nice lililokuwa likitokea Dar kwenda Masasi limepata ajali baada ya kugonga basi la Tashrif kwa nyuma na kisha kugonga magari mawili aina ya Coaster.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo la Maning nice kuovatake eneo baya na kushindwa kurudi sehemu yake. Shuhuda wa ajali hiyo ameeleza kuwa katika Coaster hiyo, watu wengi wameumia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...